Boniface Wambura.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linapenda kuwataarifu kuwa Ofisa
Habari wake Boniface Wambura ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu
la Afrika (CAF) kuwa mmoja wa maofisa watakao shughulikia masuala ya
habari wakati wa fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake
zitakazofanyika nchini Equatorial Guinea.
Uteuzi
huo umefanywa na Rais wa CAF Issa Hayatou kwa ajili ya kufanikisha
uendeshaji wa fainali hizo za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake
zilizopangwa kuanza Oktoba 28, 2012 na kumalizika Novemba 11, 2012.
Wambura atakuwa mmoja wa maofisa watatu watakaoshughulikia habari kwenye fainali hizo.
Wengine ni ofisa kutoka makao makuu ya CAF Mahmoud Garga na Arlindo Macedo kutoka Angola.
Wambura
atakuwa ni Mtanzania pekee kwenye Kamati ya Maandalizi ya fainali hizo,
kitu ambacho TFF inajivunia kutoa mwakilishi kwenye moja ya mashindanoi
makubwa ya mpira wa miguu Tanzania.
Rais wa TFF Leodegar Tenga ameelezea uteuzi huyo kuwa ni matokeo ya kazi nzuri ambayo Wambura amekuwa akiifanya tangu ajiunge na Shirikisho Januari mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment