Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiongoza ujumbe wa Tanzania
kupiga kura kuingiza agenda mojawapo kati ya agenda 5 za dharura
zilizowasilishwa kwa udharura katika mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge
Duniani (IPU) ili zijadiliwe pia. Tanzania iliungana na nchi za Afrika
kupigia kura agenda ya kujadili hali ya usalama katika nchi ya Mali
pamoja na agenda iliyowasilishwa na Uingereza kujadili kwa udharura
swala la hatma ya Usalama na Misaada wa Kibinadamu Nchini Syria na nchi
Jirani. Kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania Chini Canada Mhe. Alex C.
Massinda na Mhe. Hamad Rashid Mohamed
Spika wa Bunge akitoka katika ukumbi wa Mikutano mara baada ya
kumalizika kwa kikao cha kwanza katika Mkutano wa 127 wa Chama cha
Mabunge Duniani (IPU) mjini Quebec, Canada. Kushoto kwake ni Mhe. David
Kafulila anayehudhuria Mkutano huo pia.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na mratibu wa mahusiano baina ya Global Fund
na Mabunge Duniani Ndg. Svend Robinson, walipokutana kabla ya kuanza
kwa mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika Mjini
Quebec, Canada
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimtambulisha Mbunge wa Bunge
la Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mhe. Dr. Perpetua Nderakindo Kessy
kwa Balozi wa Tanzania Chini Canada Mhe. Alex Massinda kabla ya kuanza
kwa mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika Mjini
Quebec, Canada
Spika wa Bunge la Morocco Mhe Karim Ghellab akimkabidhi Mhe. Spika zawadi mara baada ya kufanya nae Mazungumzo
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisisitiza jambo wakati
alipokutana na Spika wa Bunge la Morocco Mhe Karim Ghellab kujadili
namna bora ya kuimarisha mahusiano baina ya mabunge ya nchi zao.
Tanzania ilipeleka ujumbe wa Wabunge kutoka kamati ya Mambo ya Nje,
ulinzi na Usalama kutembelea Bunge la Morocco Aprili mwaka huu ikiwa ni
sehemu ya kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifuatilia taarifa mbalimbali
na maazimio ya Mkutano wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa 127 wa IPU Mjin Quebec, Canada. Kushoto kwake ni
Balozi wa Tanzania Chini Canada Mhe. Alex Massinda na Mhe. Hamad Rashid
Mohamed

Ujumbe kutoka Bunge la Tanzania katika Mkutano wa 127 wa IPU
Mhe. Hamad Rashid na Mhe. Suzan Lyimo wakifuatilia kwa makini mada
kuhusu “Multilateralism and the role of parliament in parliamentary diplomacy” wakati wa mkutano huo Mjini Quebec, Canada

No comments:
Post a Comment