Lakhdar Brahimi.
Mjumbe wa kimataifa anaesuluhisha mgogoro wa Syria Lakhdar Brahimi ametoa wito kwa serikali na wapinzani wa Syria kutekeleza hatua ya kusimamisha mapigano wakati wa siku Kuu ya Eid al -Adha.
Brahimi
ametoa wito huo baada ya kukutana na Rais Bashar al- Assad mjini
Damascus, ambapo Rais Assad ameunga mkono wito huo, lakini amesema
msingi wa makubaliano lazima uwe ni wa kukomesha ugaidi.
Kwa upande wake mjumbe wa kimataifa Brahimi ametoa taarifa kuwa wapinzani ndani na nje ya Syria wanaelekea kuunga mkono hatua ya kusimamisha mapigano.
Ameeleza
kuwa hatua ya kusimamisha mapigano inaweza kuwa msingi wa kuleta
suluhisho la mgogoro wa Syria ambao mpaka sasa umeshachukua muda wa
miezi 19.
Kila siku ni mbaya zaidi kuliko nyingine. Wananchi wanauana wenyewe kwa wenyewe pamoja na kwamba wote n wa imani moja. Nyerere alisema, uhasama wa kidini dhambi yake haitaishia hapo, itaenda mpaka kabila, koo, hadi familia. Tunaomba wahusika wenye kushughulikia ambani wafanye wawezalo ili kuokoa maisha wa raia wanaoangamia kila siku hasa wanawake na watoto.
No comments:
Post a Comment