ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Monday, October 29, 2012

WAKATI MAFUTA YAKIENDELA KUPATIKANA KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA AFRIKA HUSUSAN TANZANIA, MAREKANI YAENDELEA KUVUMBUA MAFUTA YAKE NA SASA ITAKUWA YA KWANZA KWA UZALISHAJI WA MAFUTA DUNIANI


Kulingana na ripoti ya mwandishi wa masuala ya mafuta  Bwana Jonathan Fahey,  utafiti na ugunduzi wa mafuta na ggesi  Marekani unakuwa kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyoatarajiwa awali. Hii inaifanya marekani iwe nchi itakayotoa mafuta kwa wingi zaidi duniani muda mfupi ujao. Utafiti na uamuzi wa kuchimba mafuta yake mwenyewe ulifikiwa baada ya bei za mafuta na gesi kupanda sana na pia kutokana na njia mpya na za kisasa za uchimbaji mafuta hasa katiika bahari. Hii imefanya marekani kupandisha upatikanaji wake wa mafuta kwa asilimia saba mwaka huu wasani wa  galoni milioni 10.9 kwa siku. Huu utakuwa mwaka wa nne mfululizo kwa marekani kuongeza uzalishaji wa mafuta tangu mwaka 1951
Uzalishaji huu wa mafuta umeshangaza wengi hata wataalamu wa mambo ya mafuta na gesi. "Miaka mitano iliyopita kama mtu yeyote angetabiri hali hii  ya uzalishaji wa mafuta leo, watu wangefikiri ni ukichaa" amesema Jim Burkhard, mkuu wa masoko ya mafuta na utafiti wa IHS CERA kituo cha utafiti wa mafuta.
Mamlaka za mafuta na gesi za marekani zinasema kuwa, uzalishaji wa nishati hizo utakuwa kwa wastani wa  mapipa  milioni 11.4 kwa siku mwakani. Hii itakuwa ni rekodi kwa Marekani na ni chini kidogo tu ya Saudi Arabia ambayo inazalisha mapipa milioni 11.6 kwa sasa. City Bank imebashiri kuwa kiwango cha uzalishaji wa mafuta utapanda hadi mapipa milioni 13 hadi mapipa milioni 15 kwa siku ifikapo mwana 2020 hatua ambayo itasaidia kufanya Marekani kuwa "Mashariki ya Kati Mpya"
Mara ya mwisho Marekani ilikuwa iazalisha mafuta kwa wingi zaidi duniani ni mwaka 2002 baada ya Saudi Arabi kupunguza uzalishaji wa mafuta yake kwa asilimia kubwa sana kutokana na kupungua kwa bei ya mafuta baada ya shambulio la kigaidi ya 9/11. Tangu hapo Saudi Arabia na Urusi zimekuwa ndiyo wazalishaji wakuu wa mafuta duniani.
Hata hivyo pamoja na upatikanaji huu wa mafuta, Marekani bado itaendelea kuagiza mafuta kutoka nje. MArekani inatumia mafuta mapipa milioni   18.7 kwa siku. Hata hivyo Marekani imeendelea kuthibiti utumiaji usiokuwa na tija wa mafuta kwa kuweka vifaaa vinavyotumia mafuta kidogo na kwa uangalifu zaidi. Hii itafanya uagizwaji wa mafuto kutoka nje kupungua  kwa nusu ifikapo mwisho wa muongo huu. 
Hata hivyo, uzalishwaji huu wa mafuta haufanyi bei za mafuta kupungua katika soko la ndani kwa kuwa bado kuna hali ya vita katika nchi za Mashariki ya Kari na kaskazini mwa Afrika

Nitaendelea kukukusanyia taarifa za haliya uzalishaji wa mafuta na gesi kwa Tanzania na mikakati iliyowekwa na Serikaki kwa ajili ya kutumia nishati hizi kama njia ya kuliondoa taifa katika umaskini uliokithiri

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...