maiti za watoto tayari kwa kuzikwa

Waokoaji wakikimbia baada ya bomu lingine kulipuka

baada ya bomu


Mtoto aliyenusurika akipatiwa matibabu

Majeruhi wa mabomu ya Cluster

Baba akimfariji mwanaye aliyenusurika na mabomu ya Cluster

Mabomu ya Cluster ambayo yameshapigwa marufuku kutumika kutokana na athari zake kwa binadamu

Vipande viande vya Cluster bomb ambavyo bado havijalipuka
Mobu la Cluster likiwa linatoka angani tayari kwa kulipuka vipande vipande
Ndani ya bomu kubwa la cluster kunakuwa na vibomu vingine vidogo vidogo vingi na ndani ya hivyo vibomu kunakuwa na chuma nyingi mithili ya misumari hivyo kubwa likilipuka linalipua vidogo navyo hulipka na kutuma vipande vya misumari katika eneo kubwa mithili ya mvua ya mawe.

Mlipuko wa bomu la Cluster

Vibomu vya Cluster vikinyesha kama mvua ya mawe



Mlipuko wa bomu la Cluster

Bomu la cluster baada ya kufika ardhini

Wananchi wa Syria waendelea kufa kwa wingi sana. Hasi saa zaidi ya watu 40,000 wameshauwawa

Maiti hukusanywa kila siku na kuzikwa kwenye makaburi ya pamoja

Maiti zikizikwa kwenye makaburi mithili ya ya mitaro ya maji

Makaburi ya pamoja

Maiti ikibebwa baada ya kupigwa risasi

Maiti zikiandaliwa tayari kwa mazishi

kaburi la pamoja

Maiti nyingi zikikusanywa tayari kwa mazishi


Mabomu ya Cluster ambayo serikali ya Syria imekuwa ikitumia katika mapigano yanayoendelea nchini humo
Wanaharakati nchini Syria
wamesema kwamba ndege ya serikali imeangusha bomu kwenye kiwanja
wanapochezea watoto na kuwaua watoto 10.
Kanda ya video iliyowekwa katika internet inaonyesha miili ya watoto wakiwa wamelala chini huku mama zao wakiomboleza.Mapigano makali yanaendelea katika mji mkuu. Waasi waliteka sehemu moja ya kambi ya ndege za kijeshi mnamo siku ya Jumapili.
Kanda hiyo ilionyesha kile kilichoonekana kuwa mabomu madogomadogo kiwanjani. Katika kanda moja, miili ya washichana wawili ilionekana barabarani, huku nyingine ikimuonyesha mama aliyekuwa na huzuni mwingi akisimama ndani ya jengo lililoonekana kama zahanati, akiutazama mwili wa mwanawe wa kike.
Mabomu
Katika miezi ya hivi karibuni, kumekuwa na madai kila kuchao kwamba serikali ya Syria hurusha mabomu aina ya “cluster” huku mapigano yakizidi kupamba moto, ingawaje madai hayo yamekanwa na msemaji wa Serikali ya Rais Asaad.
Mabomu aina ya “cluster”, ni mabomu madogomadogo yanayounganishwa ili kutengeneza bomu kubwa.
Wanaharakati walisema kwamba mabomu mawili ya “cluster” yaliangushwa kijijini humo, huku mtu mmoja akiliambia shirika la habari la Reuters kwamba mabomu madogomadogo 70 yalipatikana.
"Wote waliouwawa walikuwa chini ya miaka 15," Abu Kassem, mwanaharakati huko Deir al-Asafir aliiambia Reuters.
Alisema watu 15 people walijeruhiwa katika shambulizi hilo, na kukana kwamba kulikuwa na wanamgambo waasi kijijini humo. Alisema walikuwepo tu viungani.
Mamia kwa maelfu ya wananchi wa Syria wameendelea kufa kila kukicha. Hata hivyo waasi wanaojiita Free Syrian Army wameendelea kufanikiwa kuteka kambi za kijeshi na mashamba a mafuta hali inayoashiria utawala wa Asaad kuelekea kuanguka muda wowote kuanzia sasa. Waasi wa Free Syrian Army wamekuwa wakipambana kumwondoa Dikteta Asaad madarakani ili kukomesha utawala wa kidikteta unaoongozwa na famililia ya Asaad uliodumu kwa miaka 40 sasa. Asaad ambaye anatoka katika kikundi kidogo cha Alawite ambacho ni sehemu ya Washia, amekuwa akiungwa mkono na Irana na wanamgambo wa Hesbollah, lakini anapingwa vikali na waislamu wa madhehemu ya Suni kama Saudi Arabi, Quarer, Quwait na Uturuki jambo ambalo limetishia kuleta vita vya ukanda wa Mashariki ya kati.
Habari na Goldentz blog na kwa msaada wa shirika la habari la Reuters
No comments:
Post a Comment