ADV
SOMA HABARI
Wednesday, December 12, 2012
ENEAGRAM SEHEMU YA 6: DOUBTER
Leo ni siku pekee zana ambapo kwa kawaida ni binadabu wachache sana watakayoiona tarehe kama ya leo. Hii ni tarehe ambayo inatokea mara moje tu katika miaka mia moja. Pasi na shaka si mimi wala si wewe tutakaokuwepo wakati tarehe 12/12/2112 (kwa kifupi 12/12/12) Hu ni ukomo na uhakika wa ufupi wa maisha yetu binadamu.
Baada ya dondoo hii ninapenda kuendelea na mtiririko wetu wa Eneagram ambapo leo ni siku ya sita na katika nafasi hii ya sita tunaongelea mtu mwenye tabia iitwayo DOUBTER/MWENYE MASHAKA MASHAKA
Huyu ni mtu mwenye ubunifu/fikra za kweli hasa juu ya chochote chenye kutishia amani na usalama wake. Anaweza kukishambulia kile kinachoweza kuwa hatari au cha kuumiza. Hivyo ni mtu anayeweza kupata woga mkubwa unaostaajabisha. Ni mtu anayehis kuwa katika hatari muda wote na huwa wa kwanza kutoa changamoto pindi hatari inapotokea. Ubunifu wake humfanya awe mchekeshaji wa kipekee. Ni mtu anayependa maisha yake yawe bila mashaka lakini anakuwa na wasiwasi juu ya watu wengine na vitu vingine vinavyomzunguka. Kila anachoambiwa na watu anakiona kama chenye makosa mengi. Hivyo watu wanaomzunguka wanamwona kama mtu mwerevu, mjuaji.. Huyu ni mtu ambaye hapendi viongozi kwa kuwa kila wanachoamua na kusema kwake ataona kuna makosa mengi. Ila cha ajabu zaidi, yeye mwenyewe hapendi kuwa kiongozi kamwe. Hapendi kuwa kiongozi kwa sababu anahisi atakuwa anaona mapungufu tu na itamwia vigumu kurekebisha kila kitu. Ni mtu aliye tayari kuwasaidia watu wanaonyimwa haki zao huku akijua kwamba yeye ni mwaminifu kabisa.
Udhaifu mkubwa wa namba 6 ni HOFU NA MASHAKA
Reflectors wake ni namba 3 na 9
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment