ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Friday, January 11, 2013

Wabunge Kenya wajizawadia mamilioni ya dola

 
Rais Kibaki akiwa Bungeni
Bunge jipya lililokarabatiwa kwa zaidi ya dola milioni kumi

  
Ukumbi wa Bunge unavyoonekana kwa nje
 
Wabunge wa Kenya wakiwa wamekaa katika moja ya vikao vyao
 
Wabunge wakifurahia baada ya mswada kupitishwa

 
Raia wa Kenya wakiandamana kupinga mishahara minono na marupurupu ya wabunge wao

Wabunge nchini Kenya wamejizawadia dola 107,000 sawa na shilingi za Kitanzania 171,200,000 (kila mbunge) kama marupurupu katika mojawpao ya vikao vyao vya mwisho vya bunge hilo kabla ya uchaguzi mkuu kufayika mwezi Machi.
Kila mbunge ataweza kupata mlinzi wa maisha, pasi ya kidiplomasia na kupata huduma za juu zaidi katika viwanja vye ndege kote duniani. Haya ndiyo mapendekezo yaliyo katika mswaada waliopiitisha ukisubiri kuidhinishwa na rais Mwai Kibaki
Ni mara ya pili wabunge wamepitisha mswaada huu wa kujizawadia mwishoni mwa vikao vyao vyabunge . Rais Mwai Kibaki alitupilia mbali mswaada wa kwanza kama huu ambao ulizua ghadhabu miongoni mwa wananchi.
Wabunge wa Kenya ni miongoni mwa wabunge wanaopokea mishahara ya juu zaidi barani Afrika kila mmoja akipata dola elfu kumi na tatu kila mwezi sawa na Shilingi za Kitanzania 20,800,000 kwa mwezi.
Lakini mshahara wa mkenya wa kawaida ni takriban dola 1,700 sawa na Tshs 2,720,000 kila mwezi.
Mswaada huu, ulipitishwa siku ya Jumatano na wabunge chini ya thelathini waliokuwa bungeni. Walikarabati bunge lao kwa kutumia dola milioni kumi na mbili kulingana na stakabadhi za bunge zilizotolewa hapo jana.
Malipo haya ni sawa na yale yaliyokuwepo katika mswaada walioupitisha mwezi Oktoba, lakini wakati huu wabunge hao pia wamependekeza marupurupu kwa rais ambaye atalipwa dola laki tatu sawa na makamu wa rais na waziri mkuu.
Alipotupilia mbali mswaada wa kwanza , Rais Kibaki lisema kuwa haiwezekani kwa wabunge kulipwa mamilioni ya dola wakati uchumi ungali umedumaa.
Tume ya kushughulikia mishahara ya wafanyakazi wa umme, iliambia wakenya kuwa hakuna uhakika ikiwa hatua yao inakuika katiba.
Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yameelezea kukerwa sana na hatua ya wabunge. Tayari waziri mkuu Raila Odinga amepinga mswaada huo akisema kuwa ni kama uhalifu dhidi ya wakenya na kwamba anashauriana na rais Mwai Kibaki kuhusu hatua itakayokuwa sawa kwa wakenya.

Habari kwa msaada wa BBC

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...