-
Wakati mkutano wa Makardinali kote ulimwenguni ukianza kwa kuwaapisha makardinali kiapo cha usiri, mwanaume mmoja aliyejulikana baadae kwa jina la Ralph Napiersi, alijaribu kuingia katika chumba cha mikutano wanapokutana hao makardinali.Hata hivyo, mtu huyo aligungulika kirahisi kwa kuwa aina ya misalaba wanayopewa makardinali inalingana kwa urefu wakati wa kwake ulikuwa mfupi kidogo. Pia mkanda unaofungwa kiunoni ulitofautiana na ule original wa makardinali. Hivyo ikawa rahisi kumnasa. Bwana huyo aliondolewa eneo hilo mara moja na walinzi wa kiswiss wanaohusika na kulinda makazi ya Vatican. Hata hivyo kwa muonekano wa haraka haraka, angeweza kuingia kwenye chumba hicho kwa kuwa alijaribu kwa kiasi kikubwa kufanana na makardinali hao.Hata hivyo baada ya kuhojiwa alieleza yeye ni Askofu wa Corpus Dei. Hata hivyo website yake ya: http://thecorpusdei.wordpress.com/the-cross/haikuwa na information za kutosheleza maelezo yake
No comments:
Post a Comment