Polisi na waokoaji wakikata bomba ili kumwokoa mtoto aliyeflashiwa chooni.
Sehemu ya bomba ambapo mtoto huyo alikwama
Uso wa mtoto huyo ukionekana akiwa katika bomba la choo
Madaktari wakihangaika kuokoa maisha ya kichanga huyo
Mtoto akiendelea kupatiwa watibabu
Mtoto aliyeokolewa chooni akiwa anapewa maziwa.
Beijing China
Wapangaji katika nyumba moja huko Mashariki mwa China walishutuliwa na mlio kama wa sungura au paka na walipoangalia ni nini waliona mguu wa mtoto mchanga ukionekana katika sehemu ya bomba la maji ya chooni. Waokoaji walijaribu kwanza kumvuta mtoto kabla hawajakata kipande cha bomba ili kumwokoa yule mtoto. Baada ya kushindwa kuchomoa kwenye lile bomba hata baada ya kulikata ilibidi wapeleke kipande cha bomba ambamo bado mtoto alikuwa amenasa, katika hospitali ya karibu iitwayo Jinhua.
Madaktari pamoja na waokoaji walijitahidi kutumia koleo na mikasi hadi kumota kichanga huyo ambaye bado hata kondo lilikuwa bado halijakatwa.
Jana mtoto huyo ambaye anajulikana kama "baby 59" alikuwa anaendelea vizuri na alikuwa akilishwa maziwa.
Maajabu ya mama wa mtoto
Mama wa mtoto huyo anatajwa na polisi kuwa na umri wa miaka 22. Polisi wanasema hadi sasa wanaamini maelezo ya huy mama ambaye yeye anadai kuwa alijirikia tumbo kumuuma ghafla na akajisikia kwenda haja kubwa. Hata hivyo siku zake za kujifungua zilishatimia. Mara mtoto akatoka wakati yeye akijisaidia hajakubwa na kutumbukia choooni
Mwanamke huyo aliwaambia maafisa wa polisi kuwa hakukusudia kutupa mtoto huyo chooni ila ilitokea kwa bahati mbaya bila yeye kujua. Hata hivyo mama huyo alijaribu kumvuta mtoto kwa kijiti akashindwa hivyo akaamua kuflash choo ili kuongoa damu lakini mtoto naye akaondoka na maji.
No comments:
Post a Comment