ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Sunday, September 15, 2013

JOHN SHIBUDA NA CCM


(Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mbunge wa CHADEMA jimbo la Maswa Magharibi Mh. John Shibuda wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Meatu mjini Meatu, ambapo ameelezea kuwa Siasa siyo ugonvi na alikuja Meatu kwa sababu mbili tu Moja ilikuwa ni kukutana na Ndugu Kinana kwa ajili ya kujadiliana mambo mbalimbali juu ya tatizo la zao la Pamba kuhusu bei ya zao hilo na matatizo ya pembejeo kwa wakulima wa Wilaya hiyo, Akongeza kwamba jambo lia pili ni kwamna Ndugu Abdulrahman Kinana ni rafiki yake wa muda mrefu kwa hata wakati wakisoma shule wote walisoma moshi Abdulrahman Kinana akisoma Old Moshi Sekondari na John Shibuda Mwenyewe akisoma Moshi Technical lakini pia akasema wakati alipokuwa akigombea ubunge wa Maswa Magharibi Kinana alimchangia shilingi Milioni moja “Siasa nia Siyo Matusi ni Ushirikiano na kukosoana kwa hoja” amemaliza Shibuda. 3 
Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi CHADEMA Mh John Shibuda akiwasili katika mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika kwenye viwanja vya Meatu mjini Meatu leo huku vijana wa Chama chaCHADEMA wakimsindikiza.. 7 
Mlemavu Daud Deus akikabidhiwa baiskeli na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika kutano wa hadhara uliofanyika mjini Meatu Simiyu leo Baiskeli hiyo imetolewa na Salim mmoja wa wana CCM wa Meatu. 15 
Daud Deus akijaribu kuendesha baiskeli yake mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana leo 16 
Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akizungumza na wanaMeatu katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Meatu leo mkoani Simiyu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...