Imechukua masaa 19 kuiamsha meli ya kifahari na ya kitajiri iitwayo "COSTA CONCORDIA" kusimama tena baada ya kulala kwenye maji kwa miezi 20 ilipogonga mwamba na kupinduka upande mmoja.
Meli hiyo inayofananafanana na ile ya Titanic ilipinduka na kuua watu 32 na wawili wakapotea hadi leo. Ni mamilioni ya dola yametumika kuinyanyua meli hiyo na sasa itapelekwa sehemu maalum kwa ajili ya kukatwa kama screpa. Maelfu ya abiria wengi wao matajiri waliokuwepo katika meli hiyo wamepoteza mali zao na mizigo yao mingi sana. Hatua ya kunyanyua meli hiyo imekuwa kivutio kikubwa sana kwa waliokuwa wakishuhudia.
No comments:
Post a Comment