Mwili wa Aisha Madinda ukitolewa kwenye gari la kubebea maiti mara baada ya kuwasili nyumbani kwao,Kigamboni.
Mwili wa Aisha Madinda ukiwasili nyumbani kwa ajili ya kuswaliwa kabla ya mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Kibada, Kigamboni jijini Dar es salaam jioni
Mwili wa Aisha Madinda ukiswaliwa kabla ya maziko huko Kigamboni jijini Dar.
WAKURUGENZI wa bendi
hasimu za dansi Tanzania, African Stars, Asha Baraka na Extra Bongo, Ali
Choki, leo wameongoza mamia ya waombolezaji kumzika aliyekuwa mnenguaji
wa zamani wa bendi hizo, Aisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’.
Mazishi ya Aisha
Madinda yamefanyika leo kwenye Makaburi ya Kijiji cha Mikwambe,
Kigamboni jijini Dar es Salaam, baada ya kukwama kufanyika jana kutokana
na zuio la Jeshi la Polisi, kupisha uchunguzi wa sababu za kifo cha
ghafla cha mnenguaji huyo.
Baada ya uchunguzi
huo kufanyika na ripoti kukabidhiwa kwa Jeshi la Polisi na familia,
mazishi hayo yakafanyika leo jioni yakihudhuriwa na Asha Baraka na
Choki, pamoja na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Salim
Omari Mwinyi.
Akizungumza katika
mazishi hayo, Asha Baraka ambaye ni Mkurugenzi wa African Stars
Entertainment inayoimiliki Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’,
alimuelezea Aisha kuwa ni sawa na mwanaye kutokana na muda mwingi
aliotumia akiwa Twanga.
Baraka aliongeza kuwa
licha ya kutokuwa na Aisha katika siku za karibuni, bado Twanga Pepeta
inatambua na kuthamini mchango wa mkali huyo wa jukwaa na kwamba pengo
lake halitasahaulika kirahisi ndani ya bendi hiyo kongwe.
Kwa upande wake Choki
alisema daima atakumbuka uwajibikaji, usikivu na upendo wa Aisha akiwa
na Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo,’ na kwamba kwake yeye marehemu ni sawa
na dada yake, huku akimtaja kama mtumishi mwema.
“Alikuwa na Extra
Bongo kwa muda mfupi, lakini aina yake ya utumishi utabaki katika
kumbukumbu zetu daima. Huu ni mwaka wa taabu kwangu, kwani siku ya
arobaini ya marehemu mke wangu, alifariki pia mzee wangu Shem Karenga,”
alisikitika Choki.
Choki alienda mbali
zaidi kwa kulalama kuwa, siku moja baada ya kumzika Shem Karenga, ndio
siku aliyofariki Aisha Madinda, hivyo kuendeleza mfululizo wa majonzi
kwake na wadau wa tasnia nzima ya muziki wa dansi nchini.
Kwa upande wake,
mtoto wa dada wa marehemu, Sheikh Mohamed Mussa, ambaye aliongoza
mazishi upande wa familia, aliwashukuru Watanzania kwa ushirikiano
walioutoa katika kufanikisha mazishi hayo, huku akiwataka kuuendelea
kumuombea.
No comments:
Post a Comment