Wakazi
waishio jirani na eneo la mauaji hayo wakiwa wamekusanyika nje ya
nyumba hiyo mjini Cairns.WATOTO nane wamekutwa wameuawa kwenye nyumba
moja katika mji wa Cairns eneo la Queensland kaskazini mwa Australia.
Vyombo vya habari nchini humo vimesema kuwa watoto hao wote kati ya miezi 18 na miaka 15 walikuwa wamechomwa visu.
Polisi wa eneo
la Queensland wanasema kuwa waliitwa kwenda kwenye nyumba hiyo baada ya
ripoti kutolewa kwamba mwanamke mmoja alikuwa amejeruhiwa vibaya. Lakini
ndani ya nyumba hiyo polisi waligundua maiti za watoto nane.
Inaaminika kuwa
watoto hao walichomwa visu hadi kufa. Polisi wanasema kuwa mtoto mdogo
zaidi kati ya watoto hao alikuwa na umri wa miezi 18 na mkubwa zaidi
alikuwa na miaka 15.
Mwanamke ambaye
anakisiwa kuwa na umri wa miaka 30 amepelekwa hospitalini akiwa na
majeraha ya visu. Ndugu mmoja wa familia hiyo aliwaambia polisi kuwa
mwanamke huyo alikuwa mama wa watoto hao.
Polisi wanasema
kuwa mama huyo hajakamatwa lakini anawasaidia kwa uchunguzi. Waziri Mkuu
wa Australia, Tony Abbott amekitaja kisa hicho kuwa uhalifu mbaya na
pia kuzitaja habari hizo kuwa za kuvunja moyo.
Polisi hawajaweza kuthibitisha ambavyo watoto hao waliuawa hadi pale uchunguzi utakapofanyika.
Wanazungumza na
watu kadhaa akiwemo mwanamume aliyeonekana karibu na nyumba hio asubuhi
na mapema, ingawa hakuna mtu yeyote amekamatwa.
CHANZO: BBC
No comments:
Post a Comment