Aliyekuwa waziri wa uchukuzi ambaye sasa ni aziri wa ushirikiano wa africa mashariki mh HARSON MWAKYEMBE akizungumza na wadau mbalimbali walojitikeza katika afla hiyo ya kutafuta fedha za kuendesha mkutano huo utakao fanyika mapema mwezi wa tatu.
Taasisi
ya kimataifa ya uhudumiaji wa bidhaa na uchukuzi wa bidhaa CILT yani THE
CHARTERD INSTITUTE OF LOGISTIC AND TRANSPORT Tawi la Tanzania imeandaa
mkutano mkubwa nchini ambao utafanyika katika mkoa wa arusha tarehe 3 na
4 mwezi wa tatu mkutano wenye lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali
wa maswala ya usafirishaji na uchukuzi kujadili changamoto mbalimbli
katika secta hiyo.
Mwenyekiti
wa CILT nchini Tanzania GEORGE MAKUKE akizungumza kuhusu mkutano huo na
taasisi hiyo inavyofanya kazi. Mkutano huo ambao utafanyika katika
hoteli ya mount meru jijini arusha una mipango pia ya kuwakutanisha
wanataaluma wa maswala ya uchukuzi na usafirishaji wa bidhaa ili
kubadilishana uzoefu katika taluma hiyo.
Akizungumza
wakati wa hafla fupi ya kupata chai yenye lengo la kuchangisha fedha
ambazo zitasaidia katika kuendesha mutano huo aliyekuwa waziri wa
uchukuzi ambaye sasa ni waziri wa ushirikian wa Africa mashariki MH
HARSON MWAKYEMBE amesema kuwa Tanzania kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa
mkutano mkubwa kama huu ni fursa ya kipekee ambayo nchi inatakiwa
kujivunia na kuitumia kujitangaza kimataifa.
Mwenyekiti
wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo ndugu ZAKARIA HANSPOP
akizngumza. Amesema kuwa mkutano huo utawasaidia hasa vijana ambao
wanasoma maswala haya kukutana na wazoefu katika fani hiyo na
kubadilishana uzoefu jambo ambalo litawajengea uzoefu katika kazi zao
pindi watakapoingia katika fani.
No comments:
Post a Comment