Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ibrahim Kilongo.
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Jeshi
la Polisi mkoani hapa limemkamata mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la
Haji Bakari (25) Mkazi wa Esso akiwa na kete 58 za madawa ya kulevya
yanayodhaniwa kuwa ni Heroine ndani ya chumba anachoishi.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP) Ibrahim Kilongo alisema kwamba tukio hilo
lilitokea tarehe 18/04/2013 muda wa saa 4:30 usiku maeneo ya Esso jijini
hapa.
Kaimu
Kamanda Kilongo alisema kwamba, mafanikio hayo yamepatikana baada ya
jeshi la Polisi mkoani hapa kupata taarifa toka kwa raia wema juu ya
kufanyika kwa biashara hiyo ndani ya nyumba moja iliyopo eneo hilo.
Alisema
mara baada ya kupata taarifa hiyo waliifanyia kazi ambapo baaadhi ya
askari waliokuwa doria walikwenda na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa
akiwa kwenye chumba chake pamoja na wenzake 12 ambao walikuwa wakitumia
madawa hayo.
“Mara
baada ya askari hao kuingia kwenye chumba cha mtuhumiwa waliziona kete
hizo zikiwa mezani huku watuhumiwa wengine wakiendelea kutumia madawa
hayo” Alisema Kaimu Kamanda Kilongo.
Mpaka
hivi sasa tayari watuhumiwa hao wameshafikishwa mahakamani leo asubuhi
mara baada ya upelelezi wa awali kukamilika ili waweze kujibu tuhuma
zinazowakabili.
Hivi
karibuni Jeshi la Polisi mkoani hapa limepata mafanikio makubwa katika
ukamataji wa madawa ya kulevya aina ya mirungi na bangi pamoja na
operesheni ya kuteketeza madawa hayo hekari kadhaa yaliyokuwa wilayani
Arumeru iliyofanyika mwanzoni mwa mwezi Machi.
No comments:
Post a Comment