ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Sunday, October 20, 2013

Mcheza wa Simba na Yanga: Mashabiki wazimia uwanjani

 Shabiki mwananke wa Yanga akitolewa kwenda kupata huduma ya kwanza baada ya kuzimia alipokuwa akishagilia bao la pili dhidi ya watani wao wa jadi Simba katika mechi ya  Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Timu hizo zimetoka sare ya mabao 3-3.

 Shabiki mwingine wa Yanga akiwa amezimia



 Wapenzi wa Yanga wakishangilioa
 Kikosi cha Yanga kilichopepetana na Simba
 
 Kikosi cha Simba kilichocheza na Yanga
 Yanga wakishangilia ushindi
 Shabiki wa Simba akiwa amezimia
 
 
Betram Mombeki alifunga la kwanza, SImba SC ikapata uhai na kurudisha yote

 SIMBA SC jana ilitoka nyuma kwa mabao 3-0 na kupata sare ya 3-3 na wapinzani wao wa jadi, Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Isarel Mujuni Nkongo, hadi mapumziko tayari Yanga SC walikuwa mbele kwa mabao 3-0.
Mrisho Khalfan Ngassa alifunga bao la kwanza dakika ya 15 akimalizia kazi nzuri ya Didier Kavumbangu aliyepiga mpira wa juu uliomchanganya kipa Abbel Dhaira na kudondokea chini kabla ya mfungaji kuusukumia nyavuni.
Betram Mombeki alifunga la kwanza, SImba SC ikapata uhai na kurudisha yote
 
Simba SC ilikuja juu baada ya bao hilo na kujaribu kusaka bao la kusawazisha, lakini walikuwa ni Yanga tena waliofanikiwa kupata bao la pili dakika ya 36, mfungaji Hamisi Kiiza aliyeunganisha mpira wa kurushwa na Mbuyu Twite.
Bao la pili lilionekana kuwachanganya Simba na kuwaacha Yanga wacheze kwa madaha zaidi, pasi nyingi za aina zote na mbwembwe za kila aina.
‘Diego wa Kampala’, Hamisi Kiiza aliifungia Yanga SC bao la tatu dakika ya 45 akimalizia pasi nzuri ya Kavumbangu, ambaye aliipasua ngome ya Simba SC na kubaki na kipa Abbel Dhaira, lakini akaamua kumpa mwenzake amfunge Mganda mwenzake.  
Kipindi cha pili, mambo yalibadilika na Simba SC wakaanza kurudisha bao moja baada ya lingine hadi kupata sare ya 3-3.
Kocha wa Yanga Brandts akilia na wachezaji wake wakati Simba SC inarudisha mabao

Hamisi Kiiza alifunga mabao mawili kipindi cha kwanza
Kipa wa Simba akishukuru mungu baada ya kusawazisha mabao matatu.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...