ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label Simba FC. Show all posts
Showing posts with label Simba FC. Show all posts

Monday, March 17, 2014

RAIS KIKWETE AMEIPA KLABU YA SIMBA FEDHA KWA AJILI YA KUKOMBOA KIWANJA.



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Jakaya Mrisho Kikwete ameipa klabu ya Simba  Sh 30 milioni kwa ajili ya kukomboa hati yao ya kiwanja cha Bunju B, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage aliwaambia wanachama wa klabu hiyo jana Jumapili katika mkutano wa wanachama wa klabu hiyo uliofanyika Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.
Rage alisema kwamba Rais Kikwete ametoa fedha hizo baada ya kufurahishwa na umoja ulionyeshwa na baadhi ya wanachama wa Simba waliojitolea kwenda katika uwanja huo kwa siku za karibuni na kufyeka majani na kuonyesha kuwa wanauhitaji.
Rage alisema alikutana na Rais Kikwete saa 2 asubuhi jana Jumapili kabla ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa Simba na kumtakia heri katika mkutano huo huku pia akitoa hundi ya Sh 30 milioni kwa ajili ya uwanja huo.
“Asubuhi leo saa 2 nilipata bahati ya kukutana na Rais Kikwete na kututakia heri katika mkutano wetu na kama unavyojua kulikuwa na matatizo ya kupata hati ya ardhi kule Bunju, tulikuwa tunadaiwa Sh 85 milioni, tulitoa milioni 50 hivyo nikamuomba Rais aingilie kati jambo hili ili kuweza kupata hati mapema na kuanza ujenzi.”
“Rais akanikabidhi hundi ya milioni 30 kama mchango wake kwetu, amedhihirisha ni mwanamichezo na mpenzi wa timu zote, kutokana na jambo hilo naamini mambo yatakwenda vizuri na zile siku 100 alizotoa katibu wa Simba  kuwa baadhi ya vitu vitakuwa vimekamilika basi vitakamilika kweli maana hadi kufikia siku hizo tutakuwa hata na sehemu ya kufanyia mazoezi timu yetu,” alisema Rage.
Aliongeza: “Kikubwa alichofurahishwa ni juhudi za wanachama kwenda kule na kuonyesha uhitaji wa uwanja na ndio maana akaamua kutoa fedha hizo ili kuhakikisha tunapata hati ya ardhi na kuanza ujenzi mara moja.”
SOURCE: MWANASPOTI

Monday, December 2, 2013

KOCHA MPYA WA SIMBA AWASILI.

a_6a71e.jpg
Mashabiki wa Timu ya Simba, wakimpokea kwa shangwe na nderemo, kocha wao mpya aliyetua nchini leo machana.
b_36c4e.jpg
Kocha huyo akikabidhiwa taji la maua na mashabiki baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.

Mara kadhaa kumekuwa kukitokea furaha kwa mashabiki, viongozi na hata wachezaji wa Klabu zetu kubwa hapa nchini, wakati wanapokuwa wanamkaribisha Kocha mpya ama kumtambulisha kwa mbwembwe nyingi, lakini anapotokea kukosea kidogo haijalishi ni muda gani amekwisha kaa na Klabu husika, anaweza kutimulia ama kuanzishiwa mizengwe hadi akakata tamaa ya kuonyesha yale yote aliyojiandaa nayo kuifanyia Klabu husika.
Wakati umefika sasa kwa Klabu zetu kufunguka kifikra na kuwa na upeo wa kufikiri ili kuziendeleza klabu zetu, kwa kuwaachia makocha waweze kufanya yale yanayostahili bila kuingiliwa na viongozi ama watu flani kwa pesa zao ama umaarufu wao katika klabu. Huko nyuma walikwishapokelewa makocha kadhaa kama alivyofanyiwa kocha huyu leo na waliondoka kimya kimya huku wengine wakiondoka klabuni kwa mafalakano na viongozi wa klabu.
c_5dc27.jpg
Akipata menu.....
d_8d6e9.jpg
Kocha huyo akiongozana na baadhi ya viongozi wa Simba wakati alipotembelea na kukagua uwanja wa mazoezi wa Klabu hiyo wa Kinesi.Picha kwa Hisani ya Lenzi ya Michezo

Sunday, October 20, 2013

Mcheza wa Simba na Yanga: Mashabiki wazimia uwanjani

 Shabiki mwananke wa Yanga akitolewa kwenda kupata huduma ya kwanza baada ya kuzimia alipokuwa akishagilia bao la pili dhidi ya watani wao wa jadi Simba katika mechi ya  Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Timu hizo zimetoka sare ya mabao 3-3.

 Shabiki mwingine wa Yanga akiwa amezimia



 Wapenzi wa Yanga wakishangilioa
 Kikosi cha Yanga kilichopepetana na Simba
 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...