ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label Simba Sports Club. Show all posts
Showing posts with label Simba Sports Club. Show all posts

Sunday, December 14, 2014

Timu ya Simba ilivyoibamiza Yanga jana.



 Emmanue Okwi akiomba dua wakati akiingia uwanjani.
 Kocha wa Simba, Patrick Phir akisalimiana na kocha wa Yanga, Marcio Maximo kabla ya mchezo. (Picha zote na
Francis Dande)
 Mgeni rasmi akisalimiana na wachezaji wa Yanga.
 Mgeni rasmi akisalimiana na wachezaji wa Simba.
Kikosi cha Yanga.
Kikosi cha Simba.
Kocha wa Yanga akitafakari.
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akiwa amenyanyua juu Kombe la Ubingwa wa mechi ya Nani Mtani Jembe msimu wa pili uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba imeshinda 2-0.

 Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Mchezo, Dk. Fenella Mukangala akimkabidhi nahodha wa Simba, Emmanuel Okwi Kombe la Ubingwa wa mechi ya Nani Mtani Jembe.

Wachezaji wa Simba wakishangilia ushindi wa timu yao.


 Umati wa mashabiki wa Yanga.

 Umati wa mashabiki wa Simba.
Mashabiki wa Simba wakiwa wamebeba mfano wa jeneza kuwakejeli watani zao.

 Beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro'

 Beki wa Yanga, Kelvin Yondan akimiliki mpira.

 Mwamuzi wa mchezo akimuonyesha kadi ya njano mshambuliaji wa Simba, Simon Serunkuma.

 Kpah Sherman akiokoa moja ya hatari langoni mwake huku Elius Maguri akimzonga.

 Mshambuliaji wa Simba Emmanule Maguri akichuana na beki wa Yanga, Nadir Haroub.

Wachezaji wa Simba wakishangilia bao lao la kwanza.

 Hassan Isihaka (kushoto) ana Ramadhani Singano 'messi' wakishangilia bao la kwanza la timu yao.

Beki wa Yanga, Oscar Joshua akimtoka Elius Maguri wa Simba.

Shabiki wa Yanga akipata msaada baada ya kuzimia jukwaani.

 Mashabiki wa Simba wakiwa na bango lenye idadi ya mabao waliyowahi kufungwa Yanga.

Leo ni 2-0.....

Burudani zikitolewa uwanjani.

 Mashabiki wakitolewa uwanjani baada ya kuzimia.
 Hali ilikuwa ngumu kwa mashabiki mpaka baadhi yao kuzimia.
Huduma ya kwanza kwa waliozimia ikitolewa.

 Beki wa Yanga, Kpah Sherman akichuana na beki wa Simba, Hassan Isihaka.

 Danny Mrwanda akiwa ameshika kichwa baada ya kukosa bao la wazi.
Ivo Mapunda akiokoa moja ya hatari langoni mwake.

 Simon Msuva akichuana na Issa Rashid.

Ivo Mapunda (katikati) akishangilia ushindi na wenzake.
Wachezaji wa Yanga wakiwa na huzuni baada ya kumalizika kwa mchezo.
Yanga wakiwa vichwa chini.

 Medali za washindi.

Monday, March 17, 2014

RAIS KIKWETE AMEIPA KLABU YA SIMBA FEDHA KWA AJILI YA KUKOMBOA KIWANJA.



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Jakaya Mrisho Kikwete ameipa klabu ya Simba  Sh 30 milioni kwa ajili ya kukomboa hati yao ya kiwanja cha Bunju B, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage aliwaambia wanachama wa klabu hiyo jana Jumapili katika mkutano wa wanachama wa klabu hiyo uliofanyika Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.
Rage alisema kwamba Rais Kikwete ametoa fedha hizo baada ya kufurahishwa na umoja ulionyeshwa na baadhi ya wanachama wa Simba waliojitolea kwenda katika uwanja huo kwa siku za karibuni na kufyeka majani na kuonyesha kuwa wanauhitaji.
Rage alisema alikutana na Rais Kikwete saa 2 asubuhi jana Jumapili kabla ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa Simba na kumtakia heri katika mkutano huo huku pia akitoa hundi ya Sh 30 milioni kwa ajili ya uwanja huo.
“Asubuhi leo saa 2 nilipata bahati ya kukutana na Rais Kikwete na kututakia heri katika mkutano wetu na kama unavyojua kulikuwa na matatizo ya kupata hati ya ardhi kule Bunju, tulikuwa tunadaiwa Sh 85 milioni, tulitoa milioni 50 hivyo nikamuomba Rais aingilie kati jambo hili ili kuweza kupata hati mapema na kuanza ujenzi.”
“Rais akanikabidhi hundi ya milioni 30 kama mchango wake kwetu, amedhihirisha ni mwanamichezo na mpenzi wa timu zote, kutokana na jambo hilo naamini mambo yatakwenda vizuri na zile siku 100 alizotoa katibu wa Simba  kuwa baadhi ya vitu vitakuwa vimekamilika basi vitakamilika kweli maana hadi kufikia siku hizo tutakuwa hata na sehemu ya kufanyia mazoezi timu yetu,” alisema Rage.
Aliongeza: “Kikubwa alichofurahishwa ni juhudi za wanachama kwenda kule na kuonyesha uhitaji wa uwanja na ndio maana akaamua kutoa fedha hizo ili kuhakikisha tunapata hati ya ardhi na kuanza ujenzi mara moja.”
SOURCE: MWANASPOTI

Tuesday, November 19, 2013

HUYU NDIYE MWENYEKITI MPYA WA SIMMBA

RageSimbaKamati ya  utendaji ya klabu ya Simba iliyokutana jana usiku imempiga stop Ismail Aden Rage kuendelea na ubosi katika klabu ya Simba na kulibadilisha benchi la ufundi isipokuwa nafasi ya meneja Madaktari wa timu ambapo pia kwa sasa wanamtarajia ZDRAVOK LOGARUSIC kutoka Croatia.
 Akizungumza kwa niaba ya kamati ya utendaji, mjumbe wa kamati ya utendaji Joseph Itangare amesema wamemsimamisha mwenyekiti kutokana na kufanya maamuzi yake binafsi bila kushirikisha kamati ya utendaji ikiwemo kutoitisha vikao vya kamati ya utendaji kwa mujibu wa Ibara ya 31 (1)ya katiba ya simba.
Kingine alichosema Itangare ni ‘vilevile mwenyekiti huyo amesaini mkataba wa kukiuuza kipindi cha Simba tv bila kushirikisha kamati ya utendaji’
Mzee Kinesi
Hii picha hapa juu ni Mzee Kinesi ambae namkariri akisema ‘kwa sasa lazima twende kikatiba, Mwenyekiti kama hayupo ngazi inayofatia inapanda juu na tunachagua Mjumbe mwingine ili kukaa kwenye nafasi iliyobakia, kwa muda huu wa matayarisho ya mkutano mkuu ujao mimi nitakaimu kama Mwenyekiti wa Simba na Swed atakaimu kama makamu Mwenyekiti’ (picha kutoka kwa salehjembe.blogspot.com)
Kwenye sentensi nyingine, Kinesi amesema ‘Mwenyekiti tumemsimamisha lakini tusubiri maamuzi ya mkutano mkuu ambao utafanyika kwa ajili ya marekebisho ya katiba, kuna mengine yamekiukwa hivyo yatawasilishwa kwenye mkutano mkuu tarehe 1 December’
‘Kutokana na timu yetu kutofanya vizuri, tumeamua kwamba benchi la ufundi tulifumue ili tulijenge upya, sasa litaongozwa na kocha aliekua na Gor MahiaZDRAVOK LOGARUSIC amekubali kuja na ataanza mazoezi tarehe 2 December na kwa pamoja tumekubaliana ndie atakua kocha mkuu, pia tumekubaliana Matola ndio awe msaidizi wake kwa muda, hatumuondoi Simba B moja kwa moja kuhofia kutetereka’

Sunday, October 20, 2013

Mcheza wa Simba na Yanga: Mashabiki wazimia uwanjani

 Shabiki mwananke wa Yanga akitolewa kwenda kupata huduma ya kwanza baada ya kuzimia alipokuwa akishagilia bao la pili dhidi ya watani wao wa jadi Simba katika mechi ya  Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Timu hizo zimetoka sare ya mabao 3-3.

 Shabiki mwingine wa Yanga akiwa amezimia



 Wapenzi wa Yanga wakishangilioa
 Kikosi cha Yanga kilichopepetana na Simba
 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...