Kufuatia kwa wafanyabiashara wa
Kariakoo kufunga maduka yao Jan 27, meneja wa taasisi ya Mkubwa na
Wanae, Yamoto Band na Wanaume Family Said Fella ameyatoa ya moyoni
kuhusiana na tukio hilo.
“Kikubwa
ni kuangalia nini tatizo maana wananchi wanasema kwamba wanaonewa kwa
hiyo Serikali ifike wakati waangalia wananchi wanaonewa kitu gani,
maanake wanasema kule wanapolipa tozo TRA kuna utaratibu wa kulipa fati
yako, la msingi wao wanachogombania kule ni kwamba biashara zote
zitumike kwa machine unakuta mtu mwingine mtaji wake mdogo anauza jeans
zake saba na shati zake kadhaa ukimwambia anunue machine laki tano au
laki tatu huo msingi wake haufanani na hizo hela za kwenda kununua hiyo
machine, kwa hiyo naomba Serikali ikae na wananchi wazungumze suala
hilo, nchi yetu ya Amani na bado tunaendelea kupenda iwe na Amani“—- Alisema Said Fela akizungumza na millardayo.com.
Hapa kuna sauti ya Said Fela akiongea na millardayo.com, isikilize kwa kubonyeza play hapa.
No comments:
Post a Comment