Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi huo.
BENKI ya CRDB imezindua kampeni maalum ya utumiaji wa huduma zake kupitia simu za mkononi 'SimBanking' kupitia kwa mawakala wa 'FahariHuduma'.
BENKI ya CRDB imezindua kampeni maalum ya utumiaji wa huduma zake kupitia simu za mkononi 'SimBanking' kupitia kwa mawakala wa 'FahariHuduma'.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kampeni hiyo ijulikanayo kama
'Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo', Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
hiyo, Dk. Charles Kimei alisema lengo la kuanzisha kampeni hiyo ni
kuwakumbusha wateja wake na watanzania wote kwa ujumla umuhimu wa
kutumia njia hizo mbadala ili kupata huduma kwa urahisi na uharaka.
Alisema
kampeni hiyo inatarajiwa kutoa magari kumi na mbili ambapo kila mwezi
mshindi mmoja atazawadiwa gari hilo, pamoja na zawadi ya gari la wateja
watakaotumia huduma hizo pia wataweza kujishindia zawadi nyingine
mbalimbali zikiwemo solar power, tables na simu za kisasa za mkononi.
"Tunataka
kuwavutia wateja wetu kuziamini na kuzitumia zaidi huduma hizi kwani ni
sawa kabisa na kupata huduma kupitia matawi yetu,".