Balozi
wa Tanzania nchini Marekani, Leberata Mulamula akiwa na Rais wa Marekan
Barack Obama mara baada ya kukabidhi hati za utambulisho Alhamisi Julai
18, 2013 katika Ikulu ya marekani "White house" na kisha kufuatia na
tafrija ya kumpongeza iliyofanyika katika ubalozi wa Tanzania nchini
Marekani.Picha kwa hisani ya Swahili Tv
ADV


SOMA HABARI

Showing posts with label President Obama. Show all posts
Showing posts with label President Obama. Show all posts
Monday, July 22, 2013
Friday, May 17, 2013
Rais Barack Obama Kutembelea Tanzania Mwezi ujao
Rais Barack Obama
Rais Barack Obama wa Marekani anatarajia kuanza ziara yake ya pili katika bara la Afrika mwishoni wa mwezi June, ziara ambayo itamfikisha Africa ya Kusini, Tanzania na Rwanda.
Katika ziara yake hiyo, atapitia Nigeria na kuongea na rais Goodluck Jonathan pamoja na waandamizi wa serikali ya Nigeria.
Mpango wa awali ulikuwa kwamba rais Obama angetembelea Nigeria kwa siku mbili lakini kutokana na hofu ya usalama kutoka kwa magaidi wa Boko Haram Nigeria inaonekana kwamba itashindwa kutoa ulinzi wa kutosha wa rais huyo wa Marekani hivyo atalazimika kukaa Nigeria kwa muda mchache.
Habari kutoka Ikului ya White House zinadokeza kuwa usalama utazingatiwa sana katika ziara hiyo na kama kutakuwa na sababu yeyote ya kuwa na wasiwasi juu ya usalama wa Rais Obama basi ziara hiyo itakatizwa wakati wowote katika nchi ya Nigeria.
Mwaka 2009 Obama alitembelea Africa na alichagua nchi ya Ghana ambapo alikutana na Raisi (marehemu) John Atta mills, na akatoa hotuba katiba bunge la Ghana na kisha kutembelea Cape Coast Castle sehemu ambapo watumwa wa Trans Atlantic walikuwa wanapakiliwa kupelekwa Marekani wakati wa biashara ya utumwa.
Kwa sis watanzania, ziara hii ya kiongozi mkubwa duniani ina manufaa gani kibiashara, kiuchumi, kiusalama? Kuna fursa gani kwa Watanzania kama ilivyoluwa kwa Rais wa China? Ni matumaini yetu kuwa ziara hii itazidi kuliweka Taifa letu katika sura nzuri kimataifa na kitaifa. Ikumbukwe kwamba, Marais wa nchi kubwa kama Marekani wanachagua kutembelea nchi zile zinazofanya vizuri katika utawala bora, demokrasia madhubuti, uhuru wa haki za binadamu, uhuru wa vyombo vya habari, kusimamia na kutimiza vyema malengo ya millenium..... Hivyo kwa Tanzania kupata ugeni kama huu ni ishara nzuri na chachu ya kuendelea kufanya vizuri zaidi. Mungu Ibariki Tanzania
Subscribe to:
Posts (Atom)