
Rais Obama akiwa na wanaye Sasha na Malia katika duka la vitabu kusupport biashara ndogo
Jumamosi ya baada ya ‘Thanks giving day’ kwa Marekani, hufahamika kama ‘small Business Saturday’, hivyo Obama kama kiongozi wa taifa hilo aliamua kuwa mfano kwa raia wa Marekani kuwaunga mkono wafanyabiashara wadogo wanaotoa huduma kwa jamii.

Wateja pamoja na wafanyakazi wa duka hilo la vitabu walipata
mshituko kumuona kiongozi wa taifa hilo kubwa na lenye nguvu duniani,
akiingia dukani hapo akiwa amevalia mavazi ya kawaida (casual), na
kuchagua vitabu kisha kwenda counter na kulipa kama wafanyavyo wateja wa
kawaida.

-Hapa Rais Obama akiwasalimia wateja aliowakuta dukani hapo

Rais Obama alionekana kujichanganya na wateja wengine na kuzungumza nao na kufurahi huku akiendelea kufanya manunuzi ya vitabu.


-Obama akilipia vitabu alivyochagua dukani hapo kama mteja wa kawaida

Baada ya kufanya manunuzi yake, Obama aliwaaga wateja na
wafanyakazi nakuwatakia “great holiday,” kisha wote wakampigia makofi.
Mke wa Rais Obama, Michelle Obama hakuwa pamoja na familia yake wakati
huo.

Baada ya kutoka katika duka hilo baadaye alitweet