HABARI
zilizotufikia mda huu zinasema Jeshi la Polisi Mkoani Dar es Salaam
limetumia nguvu kwa kurusha mabomu ya machozi ili kuwatawanya
wananchama cha Wananchi CUF waliokuwa kwenye maandamo wilaya ya Temeke .
Na
kufanikiwa kuwatia nguvuni viongozi waandamizi wa chama cha Wananchi
CUF,wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa Ibrahimu
Lipumba,huku wananchi wa maeneo hayo wakiishi kwa hofu kubwa sana.
Akithibitisha
kukamatwa viongozi hao pamoja na kuvunjwa kwa maandamano .Afisa Habari
wa chama cha Cuf ,Bwana Silas alipoongea na mtandao huu mda huu ambapo
amesema waalianza maandamano ya Amani katika Viwanja vya temeke na
kwenda mbagala , ambapo maandamano hayo yaliokuwa na lengo la
kumbukumbu ya mauaji ya wanachama wao yaliofanyika TAREHE 26 januari
mwaka 2001 huko Zanzibari na Tanzania Bara,
Bwana Silas alisema wakati wapo kwenye maandamo hayo walipofika maeneo
ya Mtongani iliyopo wilaya ya Temeke ndipo Jeshi la polisi likafika na
kurusha mabomu na kuwapiga wanachama wa chama hicho na kufanikiwa
kuwakamata viongozi wa chama hicho,na kuwapeleke kituo kikuu cha
polisi.kwa madai maandamano hayo hayana ruhusa.
No comments:
Post a Comment