ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label CUF. Show all posts
Showing posts with label CUF. Show all posts

Tuesday, January 27, 2015

BREEKING NEWS, MABOMU YATAWALA MBAGALA, PROFESA LIPUMBA AKAMATWA, NI MAANDAMO YA CUF


HABARI zilizotufikia mda huu zinasema Jeshi la Polisi Mkoani Dar es Salaam limetumia nguvu kwa  kurusha mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchama cha Wananchi CUF waliokuwa kwenye maandamo wilaya ya Temeke .
Na kufanikiwa kuwatia nguvuni viongozi waandamizi wa chama cha Wananchi CUF,wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa Ibrahimu Lipumba,huku wananchi wa maeneo hayo wakiishi kwa hofu kubwa sana.
Akithibitisha kukamatwa viongozi hao pamoja na kuvunjwa kwa maandamano .Afisa Habari wa chama cha Cuf ,Bwana Silas  alipoongea na mtandao huu mda huu ambapo amesema waalianza maandamano ya Amani katika Viwanja vya temeke na kwenda mbagala , ambapo maandamano hayo yaliokuwa na lengo la kumbukumbu ya mauaji ya wanachama wao yaliofanyika  TAREHE 26 januari mwaka  2001 huko Zanzibari na Tanzania Bara,
        Bwana Silas alisema wakati wapo kwenye maandamo hayo walipofika maeneo ya Mtongani iliyopo wilaya ya Temeke ndipo Jeshi la polisi likafika na kurusha mabomu na kuwapiga wanachama wa chama hicho na kufanikiwa kuwakamata viongozi wa chama hicho,na kuwapeleke kituo kikuu cha polisi.kwa madai maandamano hayo hayana ruhusa.

Thursday, September 26, 2013

VYAMA VYA UPINZANI VYAENDELEA NA MKUTANO WA KATIBA MPYA ZANZIBAR HAPO JANA


Mshikamano: Wenyeviti wa vyamba vya upinzani nchini wakishikana mikono kuonyesha mshikamano kabla ya kuanza mkutano kwenye Uwanja vya Kibandamaiti, Zanzibar jana.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (kushoto) akiteta jambo la Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Joseph Mbatia wakati wa mkutano wa kuungwa mkono na wananchi katika upatikanji wa katiba mpya.
Umati: Wananchi waliohudhuria mkutano huo wa kutafuta katiba mpya.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akihutubia wananchi wakati wa mkutano wa kuungwa mkono na wananchi katika upatikanaji wa katiba mpya.
Lipumba akisalimiana na Mbowe.Kwa hisani ya Global Publishers Blog

Monday, September 16, 2013

Wenyeviti wa vyama vya upinzani wakiwa pamoja, na kwa sauti moja.

 

Wenyeviti wa vyama vya upinzani wamekaa pamoja wakipinga muswada wa katiba usipitishwe. Wakuu hao wa vyama mbalimbali vya siasa na wenye ushawishi mkubwa kwa wamanchi wanakutana pamoja kwa jambo moja tu huku kila mmoja akiwa na tofauti na mwenzake. Watasimama pamoja katika hili la katiba lakini wametofautiana kwa mengi na kila mmoja wao ana nia ya kushika hatamu za uongozi wa nchi hii ya Tanzania. Kama wanavyoungana kwa ajili ya kuupinga mswada wa katiba basi wangewekeza kwenye kuondoa tofauti zao ili waungane kwenye uchaguzi. Wote wasarende uongozi wao na katiba zao wachague uongozi mpya wa muungano waweke mgombea mmoja wa urais. Wakifanya hivi naamini watakuwa wanawatendea haki Watanzania na wapiga kura watakuwa na wakati mzuri wa kuchagua viongozi bora na Wananchi wengi watajitokeza kupiga kura kwa kuwa kutakuwa na ushindani wa ukweli. Tutaingia kwenye kupiga kura bila kuwa na uhakika ni nani ataibuka mshindi, na atakayechaguliwa atakuwa anawakilisha wananchi wote.  Utengano wa wanasiasa ndio unaofanya wapiga kuwa wawe wachache. Pengine kupiga kura inakuwa kama si jambo la kishindani, unajua atakayeshinda anatoka chama fulani, so uchaguzi unakuwa kama ushahidi tu. Hii inasababishwa na ubinafsi wa vyama vya upinzania. Tupeni haki ya Demokrasia na sio kututengatenga kadiri mnavyotaka.

Saturday, July 13, 2013

CHADEMA RED BRIGED NI LAZIMA IANZISHWE...MBONA CCM NA CUF WANA KUNDI LAO



 BENSON
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema hakitarudi nyuma katika mpango wa kutoa mafunzo ya ukakamavu kupitia kikundi chake cha red brigade.
Chama hicho kimesema, tayari Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), vyote vikiwa miongoni mwa `vyama vikubwa nchini’, vina vikundi vya aina hiyo.

  Mkurugenzi wa Oganizasheni na Mafunzo Chadema, Singo Benson, ametoa msimamo huo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
Tamko la Chadema kuanzisha mafunzo hayo, limeibua taharuki na kusababisha watu kadhaa akiwamo Rais Jakaya Kikwete, kutaka mpango huo usitishwe.

LENGO LA MAFUNZO

Benson alisema lengo la kuimarisha kikundi hicho, ni kujikinga dhidi ya mashambulizi yanayoelekezwa kwa viongozi, wanachama na wafuasi wake, ambapo CCM ikitajwa kuwa nyuma ya mashambulizi hayo.

Alisema Chadema, imekamilisha maandalizi ya mafunzo yatakayowajumuisha zaidi vijana, ili wapate mbinu za kujikinga na kuwalinda viongozi wao ikiwa ni pamoja na katika mikutano ya hadhara.

Hata hivyo, alisema mpango huo hauhusishi mafunzo ya kijeshi, akidai kwamba mafunzo kama hayo yanatolewa kwa vijana kupitia kambi maalum zinazoratibiwa na CCM.

MAKAMBI YA CCM

Benson alidai kuwa kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa Igunga mkoani Tabora mwishoni mwa 2011, CCM iliandaa makambi mbalimbali ya kufundisha vijana mbinu za kijeshi.

“Iweje Chadema tuambiwe kuwa ni haramu kwa mwaka huu, wakati mwaka jana vijana wa CCM walifanya mafunzo na paredi ya jeshi ambayo ni hatari kwa nchi,” alihoji.

Alidai kuwa moja ya matokeo ya kambi za vijana wa CCM kule Igunga, ni kupigwa hadi kuuawa kwa Mbwana Masoud na Msafiri Mbwambo waliotokea Arumeru Mashariki.

Alidai kuwa matukio hayo yanajulikana hadi kwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.

AMGEUKIA MWIGULU

Benson alisema IGP Mwema anatakiwa kuanza kuwashughulikia Mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba, kwa madai ya kuwa mmoja wa waasisi wa kuwabebesha vijana silaha za kwenda kushambulia raia wasiokuwa na hatia.

Hata hivyo IGP Mwema aliliambia gazeti hili jana kwamba atatoa tamko kuhusiana na sakata hilo Jumatatu ijayo.

“Kikwete (Rais Jakaya Kikwete) awaeleze hao vijana wa CCM wanafanyaje hayo mafunzo yao, na wamekuwa wakitumika kuwapiga viongozi wa Chadema mbele ya polisi na hakuna hatua zinazochukuliwa,” alisema.

Benson alisema kabla ya polisi kuanza kuwashughulikia Chadema, wanapaswa kuanzia CCM.

“Sasa Rais Kikwete aseme hao ni wajasiriamali ama wanajeshi, na kama ni wajasiriamali bunduki walizo nazo ni za nini,” alihoji Benson.

Hata hivyo, alisema kikundi chao walichokianzisha kipo kwa mujibu wa kikatiba na kwamba watafundishwa kulinda haki za Watanzania, kuwalinda viongozi na mikutano ya Chadema.

Alisema mafunzo ya kuimarisha kikundi cha ulinzi cha Chadema yatanza wiki ijayo katika mikoa mbalimbali.

Pia, Benson alisema leo, Chadema wanatarajia kuzindua msimamo wa chama kuhusu rasimu ya Katiba Mpya katika Shule ya Msingi ya Ukombozi iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam.

UVCCM NAO WAIBUKA

Kwa upande wake, Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), imeshutumu hatua ya Chadema kuanzisha mafunzo kwa kikundi hicho cha ‘Red brigade’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,  Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigela, alisema kuwa wana wasiwasi na mafunzo yatakayotolewa na Chadema, yatakuwa na ‘sura ya kigaidi’ kwa vile yatafanyika kwa siri.

 “Tunalaani  vikali mafunzo hayo, hayana tija yoyote kwa jamii yeyote,” alisema Shigela.

Kwa mujibu wa Shigela, UVCCM haifanyi kazi za ulinzi kama `red brigade’ badala yake wanaangalia ni jinsi gani vijana wanaboreshewa huduma mbalimbali za kijamii kupitia siasa.

WAISEMEA KATIBA MPYA
Shigela aliipongeza rasimu ya Katiba Mpya kupitia Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba, kwa kuwaandaa wabunge wenye umri mdogo, tofauti na ilivyokuwa awali.

“Rasimu ya Katiba Mpya inaainisha kwamba wagombea nafasi za ubunge wanatakiwa kuwa na umri wa miaka 21 hadi 25,ila awe anakidhi kiwango na sifa za ubunge, hili ni jambo jema”, alisema.

Friday, April 26, 2013

PROFESA LIPUMBA AIPONDA CHADEMA NA KUDAI KUWA NI VINARA WA VURUGU NA HAWANA HOJA


Chama Cha Wananchi (CUF), kimesema vurugu zinazoendelea bungeni zinasababishwa na Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kushindwa kujenga hoja na mbinu za kuwabana wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema wabunge wa Chadema wana tabia ya kufuata mfumo wa kwenda bungeni na hoja zinazobeba chama chao na si za Watanzania wote kama jinsi CCM wanavyofanya.


“Kambi rasmi ya upinzani imepoteza uwezo wa kujenga hoja za mashiko na mbinu madhubuti za kuwabana wabunge wa CCM bungeni na badala yake Chadema, wamekuwa na tabia mbaya ya kubeba chama chao,” alisema Profesa Lipumba.



Alisema kambi rasmi ya upinzani pia imeshindwa kulinda utaratibu mzuri wa kutetea masilahi ya umma bila jazba na hoja zenye mashiko kama ilivyokuwa miaka ya nyuma ilipokuwa ikiongozwa na CUF, Kiongozi huyo alisema kambi ya upinzani inapaswa ijipange upya kwa utaratibu na mikakati mizuri ya kuteta hoja za wananchi bila kuyumbishwa na wabunge wa CCM.


“Bunge usiwe uwanja wa kuonyesha mbwembwe za chama bali uwe uwanja wa kutetea haki za wananchi, wabunge wanapaswa wabadilishe mitazamo ya kuona bungeni ni sehemu ya kujionyesha kisiasa na chama chako kinafanya nini nje ya Bunge,” alisema Lipumba.



Alisema viongozi wa Serikali wanapaswa kubadilika kuhusu namna ya kutoa majibu bungeni.


Profesa Lipumba alisema mawaziri wengi wanakuwa wakitoa majibu mepesi katika maswali ya msingi yanayoulizwa na wabunge wa upinzani.


Alisema Bunge linatumia muda na pesa za walipakodi vibaya kwa baadhi ya wabunge kuwa na ubishi usiokuwa na tija, kutoleana matusi na wengine kuingilia hoja za wenzao bila sababu za msingi.


Profesa Lipumba pia alisema Spika wa Bunge, Anne Makinda amepoteza uwezo wa kuliongoza Bunge.


Mwananchi
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...