ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label Mangwea. Show all posts
Showing posts with label Mangwea. Show all posts

Wednesday, June 5, 2013

Shughuli za kutoa heshima za Mwisho kwa Msanii MAREHEMU ALBERT MANGWEA zinaendelea katika viwanja vya Leaders.

 Gari lililobeba Mwili wa Marehemu Albert Mangwea likiwa limeshawasili katika viwanja vya leaders tayari kwa wakazi wa jiji la Dar kutoa Heshima zao Za Mwisho Kabla ya Mwili Kusafirisha Mkoani Morogoro kwaajili ya Mazishi
 Baadhi ya Ndugu, Jamaa na Marafiki pamoja na wana kamati wakijiandaa kuteremsha jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Albert Mangwea katika viwanja vya Leaders muda huu aliyefariki hivi karibuni Nchini Afrika Kusini
Baadhi ya Ndugu, Jamaa na marafiki wa karibu sana na Marehemu Albert Mangwea wakiwa katika sura za majonzi katika viwanja vya Leaders muda huu
 Hapa ndipo jeneza la Marehemu Albert Mangwea ndipo litakapowekwa wakati wa kutoa heshima za mwisho



                            

Tuesday, June 4, 2013

MWILI WA ALBERT MANGWAIR WAWASILI UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MWALIMU JULIUS NYERERE. VILIO NA MAJONZI VYATAWALA


Mwanamuziki kutoka kundi la wateule akiwa ameshiba msalaba wa Albert Mangwair baada ya mwili wake kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl.Julius Nyerere.



 .
 Mmoja wa marafiki na msanii Mangwair Banana Zorro akihojiwa na mwandishi wa habari wakati wakiusubiria mwili wa marehemu huyo.

 Pichani ni baadhi ya Watanzania wakiusubiria mwili wa marehemu Albert mangwair kuwasili uwanja wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere
 
 



Monday, June 3, 2013

Mwili wa msanii wa kizazi kipya aliyefariki majuzinchini afrika ya kusini marehemu Albert Mangwear kuwasili Kesho Jijini Dar es Salaam


Wadau wa Sauzi wakiwa katika harakati za kuusafirisha mwili wa msanii wa kizazi kipya aliyefariki majuzi marehemu  Albert  Mangwear jioni hii huko  Johannesburg, Afrika Kusini. Ratiba zinaonesha mwili huo utawasili kesho jijini Dar es salaam. Muda na ratiba kamili zitafuata punde

Sunday, June 2, 2013

MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWEA HAUTAWEZA KUFIKA LEO JUMAPILI



Kamati ya msiba tunaomba kutoa taarifa kwamba mwili wa marehemu ndugu yetu Albert Mangwair hautafika siku ya Jumapili ya tarehe 02/06/2013 kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali,hii ni kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu.
Kwa sasa tunasubiri taarifa kamili kutoka kwa wawakilishi 
waliopo Afika Kusini,maratutakapopata taarifa hizo tutawafahamisha zaidi.
Tunaomba radhi kwa watanzania wote kwa usumbufu wote uliojitokeza..tuendelee kuvumilia

 

Friday, May 31, 2013

Kinachodaiwa kumuua Msanii Mangwea hiki hapa


mwanamuziki marehemu Albert Mangwea 



Dar es Salaam. Wakati mazishi ya mwanamuziki marehemu Albert Mangwea(28) maarufu kama `Ngwair’ yakitarajiwa kufanyika mjini Morogoro, maeneo ya Kihonda baada ya mwili kuwasili nchini, hospitali iliyomfanyia vipimo imethibitisha kuwa pombe na dawa za kulevya kupita kiasi ndivyo vilivyomuua.
Mwili wa mwanamuziki huyo, ambaye alitamba kwenye miaka ya 2000 na wimbo wa `Mikasi’, unatazamiwa kuletwa (leo) nchini na kuagwa Jumamosi kabla ya kusafirishwa kwenda kwao Kihonda, Morogoro kwa mazishi.
Kwa mujibu wa taarifa Mangwea alifariki dunia juzi kwenye Hospitali ya St Hellen, iliyopo Johannesburg, Afrika Kusini alikokuwa amekwenda kwa shughuli za muziki.
Kifo chake
Ripoti iliyochapwa na mitandao mbalimbali ya ndani na nje ya nchi inasema marehemu alifikwa na umauti baada ya kulewa kupindukia, kibaya zaidi alikuwa hajala.
Siku ya kifo chake, Mangwea alianguka nyumbani kwa rafiki zake akiwa katika hali hiyo ya kulewa sana.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, baada ya kufikishwa hospitalini, Mangwea aligundulika kulewa mara tano ya kipimo cha kilevi kilichopitishwa na serikali ya Afrika ya Kusini, ambacho ni 416mg za pombe kwenye kila milimita 100(kwa mlevi anayeendesha chombo cha moto).
Pia marehemu alikutwa na upungufu wa hewa ya oksijeni kwenye seli na tishu za mwili wake.
Ripoti hiyo ilibainisha kuwa Mangwea, maarufu Ngwair, alikuwa na tatizo la kutokula chakula vizuri kabla ya kifo chake na pia kukosa muda wa kupumzika.
Sampuli zilizopatikana mwilini mwake zinaonyesha mkusanyiko wa dawa za kulevya mbalimbali zikiwemo heroine, cocaine chafu na bangi ya gramu 0.08 ambavyo vilikutwa kwenye damu yake.
Kifo chake kilitokana na mshtuko wa moyo na kushindwa kupumua, hali iliyosababisha mapigo ya moyo wake kusimama kwa sekunde chache, na kusababisha kifo chake.
Mwili wa Ngwair ulionekana kana kwamba alitokwa na damu nyingi puani baada ya kuonyeshwa kwa Watanzania wengi jana jioni Johannesburg, Afrika Kusini.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...