ADV


SOMA HABARI

Showing posts with label Albert Mangwea. Show all posts
Showing posts with label Albert Mangwea. Show all posts
Saturday, June 8, 2013
Thursday, June 6, 2013
M2 THE P AMUAGA RAFIKI YAKE ALBERT MANGWEA MJINI MOROGORO
M2 THE P
amefanikiwa kutoa salamu zake za mwisho kwa rafiki yake kipenzi
ambaye alikuwa naye huko Afrika kusini tena walikuwa ndani ya
chumba kimoja kabla ya mauti kumkuta Ngwea..Mwanzoni, M 2 THE P
alikuwa amefichwa na kudanganywa kuwa Ngwea alikuwa ametangulia
Tanzania. Baadaye Maggie alilazimika kumweleza ukweli .http://audifacejackson.blogspot.com.....


Rafiki wa wa karibu wa marehemu Albert Mangwea aliyekuwa amelazwa nchini Afrika Kusini amerejea Tanzania na yuko njiani akielekea mkoani Morogoro kwaajili ya kushiriki mazishi ya swahiba wake Mangwea jioni ya leo (June 6).Akizungumza na Times Fm asubuhi hii Mgaza Pende a.k.a M 2 The P amewashukuru watanzania kwa kumuombea japo hali yake bado haijawa nzuri sana lakini ameamua kurudi Tanzania kuja kumzika ndugu yake Mangwea. “Ndugu zangu watanzania mimi ni Mgaza Pende M 2 The P nawashukuru sana kwa kuniombea mpaka muda huu, nimeweza kuwasili Tanzania salama na tutakuwa pamoja kwenda kumzika ndugu yangu kipenzi changu Albert Mangwea, nawashukuru sana watanzania kwa kuniombea asanteni na endeleeni kuniombea hali yangu bado haijawa nzuri zaidi, asanteni,” alisema. Msikilize hapa

HILI NDILO kABURI LA MAREHEMU ALBERT MANGWEA
Wednesday, June 5, 2013
Shughuli za kutoa heshima za Mwisho kwa Msanii MAREHEMU ALBERT MANGWEA zinaendelea katika viwanja vya Leaders.
Gari
lililobeba Mwili wa Marehemu Albert Mangwea likiwa limeshawasili katika
viwanja vya leaders tayari kwa wakazi wa jiji la Dar kutoa Heshima zao
Za Mwisho Kabla ya Mwili Kusafirisha Mkoani Morogoro kwaajili ya Mazishi
Baadhi
ya Ndugu, Jamaa na Marafiki pamoja na wana kamati wakijiandaa
kuteremsha jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Albert Mangwea katika
viwanja vya Leaders muda huu aliyefariki hivi karibuni Nchini Afrika
Kusini
Baadhi
ya Ndugu, Jamaa na marafiki wa karibu sana na Marehemu Albert Mangwea
wakiwa katika sura za majonzi katika viwanja vya Leaders muda huu
Hapa ndipo jeneza la Marehemu Albert Mangwea ndipo litakapowekwa wakati wa kutoa heshima za mwisho
Tuesday, June 4, 2013
Vurugu zatokea wakati wa kuupeleka Mwili wa Ngwair Muhimbili Hospital
![]() |
Wananchi wamepora msalaba na kuzuia gari lililobeba mwili wa marehem |
![]()
<br>
|
FidQ akiendelea kuongoza msafara kwenda muhimbili! Watu bado wanazuia gari kuondoka |
![]() |
Wananchi wamelizunguka gari lililobeba mwili wa marehemu!! |
![]() |
Wananchi wanashusha wasanii kubeba msalaba sasa wameshusha |
![]() |
Hali ndo kama hii barabani kwenye msafara uliopokea mwiri wa marehemu |
![]() |
vurugu zimeanza after police kutokea |
![]() |
Vurugu zimezidi!! P_Majani anasaidia kuongea na police![]() Hatimaye Mwili wa Marehemu Albert Mangwea wawasili Muhimbili kwa ajili ya kuhifadhiwa hadi kesho |
MWILI WA ALBERT MANGWAIR WAWASILI UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MWALIMU JULIUS NYERERE. VILIO NA MAJONZI VYATAWALA


.
Mmoja wa marafiki na msanii Mangwair Banana Zorro akihojiwa na mwandishi wa habari wakati wakiusubiria mwili wa marehemu huyo.
Pichani ni baadhi ya Watanzania wakiusubiria mwili wa marehemu
Albert mangwair kuwasili uwanja wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere
Monday, June 3, 2013
Mwili wa msanii wa kizazi kipya aliyefariki majuzinchini afrika ya kusini marehemu Albert Mangwear kuwasili Kesho Jijini Dar es Salaam

Wadau
wa Sauzi wakiwa katika harakati za kuusafirisha mwili wa msanii wa
kizazi kipya aliyefariki majuzi marehemu Albert Mangwear jioni hii
huko Johannesburg, Afrika Kusini. Ratiba zinaonesha mwili huo utawasili
kesho jijini Dar es salaam. Muda na ratiba kamili zitafuata punde
Sunday, June 2, 2013
MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWEA HAUTAWEZA KUFIKA LEO JUMAPILI
Kwa sasa tunasubiri taarifa kamili kutoka kwa wawakilishi
waliopo Afika Kusini,maratutakapopata taarifa hizo tutawafahamisha zaidi.
Tunaomba radhi kwa watanzania wote kwa usumbufu wote uliojitokeza..tuendelee kuvumilia
Friday, May 31, 2013
Kinachodaiwa kumuua Msanii Mangwea hiki hapa

mwanamuziki marehemu Albert Mangwea
Dar es Salaam. Wakati mazishi ya mwanamuziki
marehemu Albert Mangwea(28) maarufu kama `Ngwair’ yakitarajiwa kufanyika
mjini Morogoro, maeneo ya Kihonda baada ya mwili kuwasili nchini,
hospitali iliyomfanyia vipimo imethibitisha kuwa pombe na dawa za
kulevya kupita kiasi ndivyo vilivyomuua.
Mwili wa mwanamuziki huyo, ambaye alitamba kwenye
miaka ya 2000 na wimbo wa `Mikasi’, unatazamiwa kuletwa (leo) nchini na
kuagwa Jumamosi kabla ya kusafirishwa kwenda kwao Kihonda, Morogoro kwa
mazishi.
Kwa mujibu wa taarifa Mangwea alifariki dunia juzi
kwenye Hospitali ya St Hellen, iliyopo Johannesburg, Afrika Kusini
alikokuwa amekwenda kwa shughuli za muziki.
Kifo chake
Ripoti iliyochapwa na mitandao mbalimbali ya ndani
na nje ya nchi inasema marehemu alifikwa na umauti baada ya kulewa
kupindukia, kibaya zaidi alikuwa hajala.
Siku ya kifo chake, Mangwea alianguka nyumbani kwa rafiki zake akiwa katika hali hiyo ya kulewa sana.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, baada ya kufikishwa
hospitalini, Mangwea aligundulika kulewa mara tano ya kipimo cha kilevi
kilichopitishwa na serikali ya Afrika ya Kusini, ambacho ni 416mg za
pombe kwenye kila milimita 100(kwa mlevi anayeendesha chombo cha moto).
Pia marehemu alikutwa na upungufu wa hewa ya oksijeni kwenye seli na tishu za mwili wake.
Ripoti hiyo ilibainisha kuwa Mangwea, maarufu
Ngwair, alikuwa na tatizo la kutokula chakula vizuri kabla ya kifo chake
na pia kukosa muda wa kupumzika.
Sampuli zilizopatikana mwilini mwake zinaonyesha
mkusanyiko wa dawa za kulevya mbalimbali zikiwemo heroine, cocaine chafu
na bangi ya gramu 0.08 ambavyo vilikutwa kwenye damu yake.
Kifo chake kilitokana na mshtuko wa moyo na
kushindwa kupumua, hali iliyosababisha mapigo ya moyo wake kusimama kwa
sekunde chache, na kusababisha kifo chake.
Mwili wa Ngwair ulionekana kana kwamba alitokwa na
damu nyingi puani baada ya kuonyeshwa kwa Watanzania wengi jana jioni
Johannesburg, Afrika Kusini.
Subscribe to:
Posts (Atom)