ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label nape. Show all posts
Showing posts with label nape. Show all posts

Thursday, March 12, 2015

Nape: Dk. Slaa ni Muongo na Mzushi aliyebobea Kiasi cha Kuitwa Dokta .........Aanika Maovu yake yote Amtaka amrudie Mwenyezi Mungu Haraka



Tarehe 08/03/2015, Dr. Wilbroad Slaa Katibu Mkuu wa Chadema kupitia kwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Ndugu Mabere Marando alitoa tuhuma kwa Serikali na kuwahusisha baadhi ya viongozi wa juu wa CCM kuwa wanapanga njama za kumdhuru Katibu Mkuu huyo wa Chadema.

Kimsingi tuhuma hizi ni za kipuuzi, lakini uongo huu usipojibiwa unaweza kugeuzwa kuwa ajenda na Chama hiki cha Chadema kwa kukosa ajenda zingine za maana. Hakuna asiyejua kuwa Chadema kwa sasa kinapumulia mashine, hivyo maneno na matendo yao kwa sasa lazima yalenge kujaribu kujinasua na balaa la kufa kwa chama chao.

Ni vizuri Watanzania wakakumbuka historia ya tuhuma lukuki zilizowahi kutolewana Katibu Mkuu huyu wa Chadema toka aanze siasa na ambazo zote zilikuja thibitika kuwa ni za uongo. Hapa nitawakumbusha baadhi.


Akiwa Singida katika kampeni za Urais za mwaka 2010,Dk. Slaa aliwatangazia wananchi mkutanoni kwamba kulikuwa kumekamatwa lori kubwa la mizigo (semi-trela) lililojazwa karatasi za kura za Urais zilizokuwa tayari amepigiwa kabisa mgombea Urais wa CCM, Dk.Jakaya Kikwete. Katika kuonyesha kwamba alikuwa na uhakika wajambo hilo, alisoma hadi namba za lori hilo na tela lake kutoka kwenye karatasi aliyokuwa ameshika mkononi, kisha akasema kuwa lori hilo lilikamatwa katika mji mdogo wa Tunduma, mkoa wa Mbeya wakati likiingia nchini kutoka Lusaka, Zambia.
Lakini baada ya polisi kuchukua hatua za haraka wakitumia namba za lori na tela lake alizokuwa amezisoma na kulikamata, kisha wakalipekua hadharani huku wananchi wakishuhudia palepale Tunduma, kilichokutwa ndani ya lori ilikuwa shehena ya vipodozi vya kina mama na sabuni za manukato.Baada ya siku chache huku akiwa amesahau yote, Dk.Slaa akatangaza tena kuwa mgombea Urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alikesha katika hoteli ya Lakairo, Mwanza akiweka mikakati ya kuiba kura siku ya uchaguzi huo wa mwaka 2010 ili ashinde. Siku chache alisema kura zimeingizwa na zimeshapigwa, hapa amesahau anadai ndio kwanza mpango unapangwa.

Aliwataja watu wengine aliodai walikuwa pamoja na Rais Kikwete kuwa ni aliyekuwa Mbunge wa Igunga,Rostam Aziz na Mkurugenzi wa Hoteli hiyo iliyopo katika jiji la Mwanza, Lameck Airo.

Lakini wakati Dk. Slaa akisema uongo huo,Rais Kikwete siku nzima na usiku wake wote alikuwa Mtwara akiendelea na kampeni zake za Urais.

Hata Rostam Aziz naye kwa siku hiyo pamoja na usiku wake wote alikuwa Igunga akiendelea na kampeni zake za Ubunge, na pia hata Airo naye siku nzima na usiku wote huo alikuwa jimboni kwake Rorya akifanya kampeni zake za kugombea Ubunge.

Baada ya kushindwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Dk. Slaa aliwaambia waandishi wa habari kwamba alikuwa na ushahidi wa matokeo ya Urais ya kituo kwa kituo ya nchi nzima yakionyesha kuwa alishinda.

Akasema, chama chake kingeyasoma hadharani na kuwakabidhi waandishi wa habari ili wananchi waujue ukweli kuwa alidhulumiwa ushindi wake, kazi iliyofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na haki yake akapewa aliyekuwa mgombea Urais wa CCM, Jakaya Kikwete.

Lakini kwa vile alikuwa akiwatangazia uongo wananchi, Dk. Slaa hadi leo hajawahi kuyasoma matokeo hayo ya kughushi, badala yake alipowaita tena waandishi wa habari akatangaza kuwa Tanzania isingetawalika mpaka arudishiwe haki yake. Hapo ndipo ghasia zikiwemo za mauaji za Chadema zilipoanza hadi leo.
Januari, 2011 aliwaambia waandishi wa habari kwamba alikuwa na mkanda unaothibitisha kuwa mauaji ya Januari 5, mwaka huo yaliyofanyika katika jiji la Arusha kutokana na maandamano ya vurugu ya wafuasi wa Chadema yalifanywa kwa makusudi na polisi, na kwamba wafuasi wake hawakufanya fujo wala vurugu zozote.

Alisema mkanda huo angeuonyesha mbele ya waandishi wa habari ndani ya siku tatu au mbili baada ya Polisi Makao Makuu,kuonyesha unaothibitisha kwamba wafuasi wa Chadema walifanya vurugu ikiwemo kutaka kuvamia Jengo la Makao Makuu ya Polisi la Mkoa na kupora silaha zilizokuwa humo, wawafungulie wahalifu waliokuwa ndani na kulichoma moto jengo lenyewe.

Lakini tokea kipindi hicho hadi sasa ikiwa tayari imeshapita miaka minne, Dk. Slaa siyo tu ameshindwa kuuonyesha mkanda huo “ndani ya siku tatu ama mbili” alizokuwa ameahidi, bali amethibitisha kwamba alichosema kwa Watanzania ulikuwa ni uongo na uzushi.
Mwaka 2011, Dr. Slaa alikwenda mbali kwa kuzusha kwenye mkutano wa hadhara kuwa aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakati huu Brig. Gen. mstaafu Yohana Balele amefariki dunia.

Akajaribu kuwaaminisha wananchi pale kuwa ni kweli, baadae ikagundulika kuwa Mkuu huyo wa Mkoa ni mzima na wala haumwi. Haikujulikana mara moja sababu za Dr. Slaa kumzushia kifo Mkuu huyo wa Mkoa.
Julai 2012, Dr. Slaa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika walizusha kwamba wanafuatiliwa na baadhi ya Maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa ili wauawe, lakini walipotakiwa kupeleka ushahidi wao katika vyombo vya dola ili kusudi watuhumiwa wachunguzwe na hatimaye wakamatwe na kuruhusu Sheria ichukue mkondo wake, wote waligoma na kudai hawapo tayari kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Waliendelea na msimamo huo hata pale Dk. Slaa alipolazimishwa kwenda Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na kuhojiwa, lakini akashindwa kutoa uthibitisho wake mwenyewe wala wa Mnyika kwa sababu walidai suala hilo limezungumzwa katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema.
Mwaka 2012, Dr. Slaa akiwa ziarani Ifakara wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro, alidai kuwa CCM imeingiza silaha kutoka nje ya nchi kontena zima, ili zitumike kuwadhuru viongozi wa Chadema, jambo ambalo hata hivyo hadi leo ameshindwa kulitolea uthibitisho wala kielelezo chochote.

Wanaomfahamu vizuri endapo ingekuwa kweli angeita waandishi wa habari, akatoa ushahidi wake na kuwakabidhi ili wautumie kuandika madai hayo, lakini kwa sababu ulikuwa ni uongo ndiyo maana hakutoa karatasi yoyote hadi leo.
Juzi bila aibu anaibuka na tuhuma zingine za eti kutaka kuuawa. Kupanga kumdhuru Dr. Slaa, ili CCM ipate nini kwa kudhurika kwake? Kwa umri wake, afya yake na kadhalika, kwa nini CCM ipange kumdhuru mzee huyu? Huu ni mwendelezo wa tabia yake ya kuzusha mambo ya uongo kila anapoona anachuja kisiasa. Ni busara kwa umri wake akatumia muda wake mwingi KUMRUDIA MWENYEZI MUNGU.



Lakini hata mtu aliyetumika kuufikisha uongo huo kwa umma, naye ana historia ya kuzusha mambo na kusema hata asiyoyaamini.

Marando aliwahi kuitisha kikao na waandishi wa habari na kudai Katibu wa Itikadi na Uenezi alifaidika na pesa za EPA, alipobanwa na mteja wake aliyekuwa akimtetea mahakamani kwa kesi hiyo hiyo ya EPA, akaruka yale matamshi yake kwa maandishi na kudai ilikuwa ni shinikizo la Chama chake kusoma yale maneno lakini hata yeye hayaamini.

Lakini ni Marando huyu huyu ambaye akipanda kwenye majukwaa ya siasa anadai swala la EPA ni ufisadi mkubwa sana kwa nchi na akishuka tu jukwaani, anakimbia mahakamani kwenda kuwatetea watuhumiwa hao hao wa EPA aliowaita majukwaani mafisadi wa EPA. Mzee huyu naye ni MNAFIKI.

Hebu tujiulize, ni lini Mabere Marando aliacha rasmi kazi yake ya awali ya ukachero mpaka aaminike leo kufanya kazi afanyayo? Nani alimtumia kujaribu kusambaratisha chama cha NCCR-Mageuzi miaka ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi nchini? Hivi ni kweli Marando ni wa kuaminiwa leo?

Natoa wito kwa Watanzania bila kuingilia utaratibu wa Sheria na vyombo vya Serikali kufuatilia uongo huu mpya, Watanzania nawaomba wampuuze na kupuuza uongo huu. Usitupotezee muda, tuendelee na mambo ya msingi ya kujenga nchi yetu.

Nimshauri pia BABU yangu Dr. Slaa, kwa umri wake, wenzake wakifikisha umri huu wa uzee wanatumia muda wao kumrejea Mwenyezi Mungu badala ya yeye kuendelea kutunga uongo na uzushi kila kukicha. Namwomba mwenyezi Mungu amuwezeshe kuiona busara hiyo.

Imetolewana:-


NapeMoses Nnauye,

KATIBUWA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADINA UENEZI10/03/2015

Monday, May 5, 2014

Kinana aunguruma Pemba


 
Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.Katika hobuba yake,Ndg. Kinana amewataka Wananchi wa Kisiwani humo,kutohadaika na Wanasiasa wanapita kila mahali kwa lengo la kulipotosha Taifa,hasa juu ya swala la Muundo wa Serikali katika Mchakato wa Katiba Mpya.
35
Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akiendelea kuwahutubia wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,Ndg. Vuai Ali Vuai akizungumza na wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika jana kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye akiwapa somo wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale, Kisiwani Pemba.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye akiendelea kuzungumza.
Makamu Mwenyekiti UWT,Bi. Asha Bakari Makame akizungumza kwa msisitizo mkubwa na wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale, Kisiwani Pemba.

Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar,Ndg. Shaka Hamdu Shaka akizungumza machache na wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.

Vijana wa CCM, Fatma Juma Ramadhan (kushoto) na Halima Juma Hajj wakighani mashairi mazuri ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana (hayupo pichani).
Sehemu ya picha mbali mbali za wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba wakifuatilia Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika jioni ya jana kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.(Picha zote na Othman Michuzi).

Thursday, December 5, 2013

Kinana amaliza ziara yake Mbeya


1
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda bajaji tayari kwa kuelekea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Luanda Nzovwe Mwanjelwa jijini Mbeya akitokea ofisi za CCM mkoa wa Mbeya, huku Nape Nnauye naye akijiandaa kuinga kwenye bajaji. Kinana akiongozana na Ujumbe wake pamoja na viongozi wa mkoa wa Mbeya na wilaya leo wametumia usafiri huo ili kuonyesha kwamba Chama hicho ni chama cha wananchi wa kawaida ambao ni wafanyakazi na wakulima tofauti na wenzetu wanaojifanya wanawatetea lakini wanakuja na Helikopta na kuwachangisha michango ya fedha kisha wanatokomea zao. Katika msafara huo pia yupo Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Mbunge wa kuteuliwa.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MBEYA) 2
Msafara ukielekea kwenye mkutano
4Vijana wa Mwanjelwa wakiuzuia msafara wa Kinana wakati alipokuwa akielekea uwanja wa Luanda Nzovwe kwenye mkutano jambo lililofanya Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye watembeee kwa mguu(P.T)
7
Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye wakitembea kwa miguu katika eneo la Mwanjelwa huku vijana wakiwashangilia 8
Abdulrahman Kinana akiwa katika bajaji iliyomchukua
9Nape Nnauye akiwa katika Bajaji iliyombeba
10Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wakiwapungia mikono wananchi wakati wakielekea kwenye mkutano. 13
Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Mbunge wa kuteuliwa akizungumza na wananchi katika mkutano huo. 14
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wengine wakiwa katika meza kuu.
17Umati wa watu waliohudhuria katika mkutano huo.
18Kada wa CCM aliyejiunga na CCM hivi karibuni akitoka chama. cha CHADEMA Braison Mwasimba akiunguruma katika mkutano huo 19
Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye akimwaga sumu katika mkutano huo.
20Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye akiwaimbisha wananchi katika mkutano huo.
22Msanii wa muziki wa kizazi Kipya Michael Senka mashairi jukwaani wakati mkutano huo ukiendelea leo jioni.
24Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akitolea ufafanuzi wa mbolea ya Minjingu ambayo imekataliwa na wananchi wa mkoa wa Mbeya huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza kwa makini
25Kada wa Chama cha Mapinduzi Tambwe Shitambala akizungumza katika mkutano huo.

Tuesday, November 19, 2013

Nape ataka CHADEMA KIFUTWE

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kukifuta Chadema kwa madai kuwa, kimeshindwa kusimamia katiba yake kwa kutofanya uchaguzi wa ndani zaidi ya miaka zaidi ya kumi.
 
Nape alisema chama hicho kimejaa viongozi waongo, wapenda vurugu na wanaotaka kuvuruga amani ya nchi kwa kisingizio cha Katiba Mpya na kwamba, wamesahau katiba iliyopo imedumu kwa miaka 50 na haijawahi kuwagombanisha wananchi wala kuwavuruga. 
Hata hivyo, jitihada za kumpata Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema, John Mnyika kuzungumzia tuhuma hizo jana jioni kwa simu yake haikufanikiwa.

Akihutubia wakazi wa Manispaa ya Songea jana, Nape alimtaka Msajili wa Vyama vya Siasa kukiagiza chama hicho kufanya mkutano wa uchaguzi haraka kikigoma akifute na kwamba, asipofanya hivyo wao wataendelea kumsema na kumchukulia hatua. Aliongeza CCM kilifanya uchaguzi wake 2012 na kupata viongozi wapya, lakini Chadema imeshindwa kusimamia katiba yake ambayo ilipeleka kwa msajili wa vyama na kuisajili kwa kuivunja wao wenyewe kwa kuendesha chama isivyo. Nape alisema chama hicho hakifai kuongoza nchi, kwani kimeshindwa kusimamia katiba yake na kuifuata hakiwezi kuongoza wananchi. 
“Kwa sababu Msajili wa Siasa ni mlezi wa vyama vyote vya siasa ikiwamo Chadema, namuomba akiagize chama hicho kifanye uchaguzi kwani wao wanajiita wanademokrasia wakati wanashindwa kufuata demokrasia kwa vitendo,” alisema Nape.
 
Kuhusu malalamiko ya wananchi, Nape alisema wananchi wamekuwa wakilalamikia utendaji mbovu wa viongozi wa Serikali na kwamba, yana msingi kwani inasikitisha licha ya Ruvuma kuwa ni mkoa unaolisha nchi, hakuna mawazili wa kilimo ambao wamefika mkoani hapa. CHANZO MWANAINCHI

Thursday, June 6, 2013

Uongozi wa CCM Wakutana Kwa Mazungumzo na Ujumbe wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam (CVP)


 .Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha katika hoteli ya Protea Cortyard jijini Dar es Salaam, Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Hoang Quan, baada ya mgeni huyo na ujumbe wake kuwasili kwa ajili ya mazungumzo na Kinana, jana, Juni 6, 2013.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha katika hoteli ya Protea Cortyard jijini Dar es Salaam, Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Hoang Quan, baada ya mgeni huyo na ujumbe wake kuwasili kwa ajili ya mazungumzo na Kinana, jana, Juni 6, 2013.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akimpa zawadi ya sanamu ya twiga iliyotengenezwa  kwa vyuma chalavu, Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Hoang Quan, wakati wa chakula cha mchana kwenye mgahawa wa Akemi, jijini Dar es salaam. Sanamu hiyo ni ubunifu unaofanywa na kikundi cha walemavu jijini Dar es salaam
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimshukuru Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Hoang Quan, baada ya mazungumzo yao katika hoteli ya Protea Courtyard, Dar es salaam, leo. Kushoto ni Dk. Asha Rose Migiro na watatu kushoto ni Nape Nnauye.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  (wapili kulia) akizungumza na Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam (CVP), Hoang Quan (wapili kulia), katika hoteli ya Protea Cortyard jijini Dar es Salaam. Jana Juni 6, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Watatu kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Hoang Quan, akizungumza katika hoteli ya Protea Courtyard, Dar es salaam, jana.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Phili Mangula akizungumza wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili ya ujumbe wa Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Hoang Quan (wapili kushoto) katika Mgahawa wa Akemi jijini Dar es Salaam.jana. Picha zote na Bashir Nkoromo
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...